Taarifa Rasmi

Miongozo ya Usalama

Ili kuwa na uzoefu mzuri na salama, tunashauri yafuatayo: Kwa Wateja: Tumia Mfumo wa Chat: Fanya makubaliano yote ya bei na aina ya kazi kupitia mfumo wetu wa Chat kabla ya kumpa kazi fundi. Hii inasaidia kuwa na ushahidi. Kutanguliza Pesa: Epuka kumpa fundi pesa yote ya ufundi kabla kazi haijakamilika na wewe kuridhika, isipokuwa pesa ya kununulia vifaa vya kazi (ambayo unashauriwa kuyanunua mwenyewe au kwenda naye dukani). Usalama Nyumbani: Kuwa makini unapomkaribisha mtu usiyemjua nyumbani kwako. Hakikisha kuna mtu mwingine wa karibu wakati kazi inafanyika. Kwa Mafundi: Kuwa Mtaalamu: Fika kwa wakati ulioahidi, na fanya kazi kwa weledi. Hii itakupa "Nyota 5" na kukuletea wateja wengi zaidi. Ulinzi Wako: Toa makadirio (Quotation) ya wazi mapema ili kuepuka usumbufu wa mteja kukataa kulipa baada ya kazi. Wasiliana: Tumia lugha nzuri kwa wateja kupitia mfumo wetu wa Chat.

Je, una maswali zaidi?

Wasiliana na ofisi zetu kwa ufafanuzi zaidi juu ya huduma zetu.