Sera ya Faragha
Ilisasishwa: Oktoba 2026
Sera hii inaeleza taarifa gani Fundi Mkononi inakusanya, kwa nini, nani anaziona, na haki zako chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022 (PDPA). Mdhibiti wa taarifa ni FUNDI MKONONI, Dar es Salaam, Tanzania.
1. Taarifa tunazokusanya
| Unayemhusu | Taarifa | Kwa nini |
|---|---|---|
| Wote | Jina, namba ya simu, password (imefichwa kwa hash), email (si lazima) | Kufungua akaunti, kuingia, kutuma kodi ya OTP |
| Mteja | Maombi ya kazi (tarehe, mahali, maelezo), ujumbe wa chat, maoni na nyota | Kumuunganisha na fundi, usuluhishi wa migogoro |
| Fundi | Huduma, bei ya kuanzia, wasifu, picha ya wasifu na za kazi, mkoa, wilaya, mtaa, eneo la GPS (si lazima), namba ya WhatsApp, namba ya NIDA (si lazima), taarifa za kampuni | Kumwonyesha kwa wateja, kuthibitisha utambulisho |
| Kibarua | Mwaka wa kuzaliwa, eneo, GPS (si lazima), kazi anazoweza, picha (si lazima) | Kumwonyesha kwa mafundi na wateja, kuhakikisha ana miaka 18+ |
| Anayelipa | Namba ya simu ya kulipia, kiasi, kumbukumbu ya malipo | Kuwasha kifurushi, hesabu za kisheria |
| Jamii | Mada, majibu, picha unazopakia, "Imesaidia" na ripoti | Kuendesha Jamii na kuisimamia |
| Kiufundi | Anwani ya IP, aina ya kifaa, kumbukumbu za usalama (mf. majaribio ya kuingia), idadi ya waliotazama wasifu | Usalama, kuzuia utapeli na spam |
Tukikuuliza GPS, simu yako itakuomba ruhusa kwanza. Eneo unalotumia kwa "Karibu nami" halihifadhiwi kwenye akaunti yako.
2. Nani anaona taarifa zako
- Kila mtu anaona wasifu wa fundi: jina, picha, huduma, eneo, bei, picha za kazi na maoni.
- Namba ya simu ya fundi inaonekana wakati Free Mode imewashwa, au baada ya fundi kukubali miadi. Namba ya WhatsApp aliyoiweka fundi inaonekana kwenye wasifu wake.
- Namba ya simu ya kibarua inatolewa kwa fundi au mteja aliyeingia tu, na kila anayeipata anarekodiwa.
- Fundi anaona jina, namba na maelezo ya kazi ya mteja aliyemtumia ombi au ujumbe.
- Jamii: mada na majibu yako ni ya umma, na yanaonyesha jina lako la kwanza na herufi ya kwanza ya jina la pili (mf. "Juma S.").
- Watoa huduma wetu wanaoshughulikia taarifa kwa niaba yetu tu: huduma ya SMS, huduma ya malipo ya simu, kampuni ya seva (hosting), huduma ya email, na Google (usambazaji wa app kupitia Google Play, na fonts za tovuti).
- Vyombo vya sheria vya Tanzania, pale tu sheria inapotutaka.
Hatuuzi taarifa zako, wala hatuzitumii kwa matangazo ya makampuni mengine.
3. Cookies
Tunatumia cookies za lazima tu: cookie ya kikao (session) ili ubaki umeingia, cookie ya eneo ulilochagua (mf. mkoa wako), na cookie inayotambua kama unatumia app. Hatutumii cookies za matangazo wala za kufuatilia watu.
4. Muda wa kuhifadhi
- Akaunti na taarifa zake: mpaka uifute.
- Ukifuta akaunti: wasifu, picha, chat, maombi, maoni, machapisho ya Jamii na kumbukumbu za mawasiliano zinafutwa. Kumbukumbu za malipo zinabaki kwa ajili ya hesabu na sheria za kodi, bila kuunganishwa na namba yako.
- Nakala za akiba (backups) za mfumo zinahifadhiwa kwa siku 7 kisha zinafutwa zenyewe.
- Kumbukumbu za usalama (IP, majaribio ya kuingia) zinafutwa ndani ya siku 90.
5. Usalama
Password zinahifadhiwa kwa hash (si maandishi ya wazi), tovuti inatumia HTTPS, namba za simu zinathibitishwa kwa OTP, na kuna vikomo vya majaribio vinavyozuia kubahatisha password. Hakuna mfumo ulio salama kwa asilimia 100. Tukigundua uvujaji wa taarifa unaokuhusu, tutaripoti kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) na kukujulisha.
6. Haki zako
Unaweza: kujua tunazo taarifa gani kukuhusu; kurekebisha taarifa zisizo sahihi (nyingi unazibadilisha mwenyewe kwenye akaunti); kufuta akaunti na taarifa zako (fundimkononi.com/futa-akaunti); kupinga matumizi fulani ya taarifa; na kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC). Tutajibu ombi lako ndani ya siku 30.
7. Watoto
Huduma hii si ya watu walio chini ya miaka 18. Tukigundua akaunti ya mtoto, tutaifuta.
8. Taarifa nje ya Tanzania
Baadhi ya watoa huduma wetu (kama seva na Google) wanaweza kuhifadhi taarifa nje ya Tanzania. Taarifa zinapohamishwa nje ya nchi, tunafanya hivyo kwa kufuata masharti ya PDPA.
9. Wasiliana nasi
Maswali kuhusu faragha: [email protected] · WhatsApp: kitufe cha WhatsApp chini ya ukurasa